Thursday, February 27, 2025

    JKT TANZANIA YATOA SARE NA KENGOLD, 1-1 MBWENI


    WENYEJI, JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kengold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali  Charles Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
    JKT Tanzania walianza kupata bao, mfungaji Edward Songo kwa penalti dakika ya 45’+6, kabla ya mshambuliaji Suleiman Salim Rashid 'Bwenzi' kuisawazishia Kengold dakika ya 85.
    Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 27, ingawa inabaki nafasi ya sita — na Kengold inafikisha pointi 15, nayo inabaki mkiani kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 22.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi y 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT TANZANIA YATOA SARE NA KENGOLD, 1-1 MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry