TIMU ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya JKT Tanzania leo yamefungwa na Hassan Nassor Maulid dakika ya 10 na Wilbroad Maseke aliyejifunga dakika ya 68.
Kwa ushindi huo, Maafande hao wa Jeshi la Kujenga Taifa wanafikisha pointi 22 na kusogea nafasi ya saba, wakiizicdi tu wastani wa mabao KMC ambayo inashuka kwa nafasi moja hadi ya tisa.
0 comments:
Post a Comment