WENYEJI, JKT Tanzania wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioninya leo Uwanja wa Meja Jenerali Michel Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na mshambuliaji Edward Songo dakika ya 40 kwa penalti na beki Wilson Nangu dakika ya 61.
Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 26 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya sita, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 15 nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 21.
0 comments:
Post a Comment