BAO la mkwaju wa penalti la Amos Charles dakika ya 27 limeipa Fountain Gate ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati mkoani Manyara.
Kwa ushindi huo, Fountain Gate wanafikisha pointi 25 na kupanda hadi nafasi ya nane, wakati Tanzania Prisons wanabaki na pointi zao 18 nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 22.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi y 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment