WENYEJI, Fountain Gate wametoka sare ya bila mabao na jirani zao, Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati mkoani Manyara.
Kwa matokeo hayo, Fountain Gate inafikisha pointi 22 na kusogea nafasi ya saba, wakati Tabora United inafikisha pointi 33 na inabaki nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi 20.
0 comments:
Post a Comment