WENYEJI, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Paul Peter dakika ya 57, Iddi Kipagwile dakika ya 64 na Augustine Samson dakika ya 90’+4, wakati ya Tanzania Prisons yamefungwa na Beno Khalfan Ngassa dakika ya 19 na Lambert Sibiyanka dakika ya 78.
Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC wanafikisha pointi 23 katika mchezo wa 19 na kusogea nafasi ya saba kutoka ya 13, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 17 za mechi 20 nafasi ya 14.
0 comments:
Post a Comment