WENYEJI, Coastal Union wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Bakari Msimu dakika ya 26 na Maabad Maulid dakika ya 68, wakati la JKT Tanzania alijifunga beki Lameck Lawi dakika ya 64.
Kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya sita, wakati JKT Tanzania wanabaki na pointi zao 19 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 17.
0 comments:
Post a Comment