WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yote leo yamefungwa na viungo, Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 29, Mkongo, Ellie Mpanzu Kibisawala dakika ya 44 na mzawa, Ladack Juma Chasambi dakika ya 45’+2.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 47 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 18.
Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 17 za mechi 18 Sasa nafasi ile ile ya 14 kwenye ligi ya timu 16.
0 comments:
Post a Comment