MABINGWA watetezi, Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya wenyeji, Mashujaa katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Mkenya, Duke Ooga Abuya dakika ya 31, mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 48, viungo — Mganda Khalid Aucho dakika ya 53 na Mzambia, Clatous Chota Chama mawili, dakika ya 74 na 83.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 55 katika mchezo wa 21 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano dhidi ya watani, Simba SC ambao pia wana mechi mbili mkononi.
Kwa upande wake, Mashujaa wanabaki na pointi zao 23 za mechi 21 pia na kuteremka kwa nafasi moja hadi ya tisa katika ligi ya timu 16.
0 comments:
Post a Comment