MABINGWA watetezi, Yanga wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Pamba Jiji FC 3-0 jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na beki Mkongo, Chadrack Isaka Boka dakika ya 28 na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki ‘Baba Hamisa’ mawili dakika ya 75 na 77.
Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 58 katika mchezo wa 22 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi saba zaidi ya mahasimu, Simba ambao pia wana mechi mbili mkononi.
Kwa upande wao Pamba Jiji baada ya kupoteza mchezo huo, inabaki na pointi zake 22 za mechi 22 katika nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment