WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo Zidane Sereri dakika ya 72 na beki kutoka Mali, Yoro Mamadou Diaby dakika ya 82.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Simba SC yenye pointi 47 za mechi 18 na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 49 za mechi 19.
Kwa upande wao Mashujaa baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki nafasi ya 10 na pointi zao 20 za mechi 19 pia.
0 comments:
Post a Comment