TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua mawili yote kwa penalti dakika ya 45 na 71, wakati lingine amefunga mshambuliaji Mganda, Steven Dese Mukwala dakika ya 90’+1.
Simba ingeweza kuondoka na ushindi mnono zaidi kama si mshambuliaji Mcameroon Christian Leonel Ateba Mbida kukosa penalti nyingine dakika ya 52.
Namungo FC ilimaliza pungufu mchezo huo baada ya beki wake Derick Mukomnozi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 33.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 50 katika mchezo w 19, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
Kwa upande wao Namungo FC baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 21 za mechi 20 nafasi y 13 kwenye Ligi ya timu 16.
0 comments:
Post a Comment