• HABARI MPYA

        Sunday, January 05, 2025

        SIMBA SC YAICHAPA SFAXIEN 1-0 TUNISIA BAO LA AHOUA


        TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, CS Sfaxien katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Olympique Hammadi-Agrebi mjini Radès nchini Tunisia.
        Bao pekee la Simba katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast Jean Charles Ahoua dakika ya 34.
        Kwa ushindi huo, Simba SC imefikisha pointi tisa na kupanda kileleni mbele ya Bravos do Marquis ya Angola na CS Constantine ya Algeria zenye pointi sita kila moja, wakati CS Sfaxien inabaki mkiani kwa rekodi ya kupoteza mechi nne, mbili nyumbani na mbili ugenini. 
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA SFAXIEN 1-0 TUNISIA BAO LA AHOUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry