TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na beki raia wa Mali, Yoro Mamadou Diaby mawili dakika ya pili na 31 na lingine mshambuliaji Msenegal, Alassane Diao dakika ya 79, wakati ya JKT Tanzania yamefungwa na Edward Songo dakika ya 48 na Abdurahman Bausi dakika ya 90’+6.
0 comments:
Post a Comment