// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA YACHAPWA 2-0 TENA LIGI YA MABINGWA AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA YACHAPWA 2-0 TENA LIGI YA MABINGWA AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 08, 2024

    YANGA YACHAPWA 2-0 TENA LIGI YA MABINGWA AFRIKA


    WENYEJI, MC Alger wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika usiku wa Jumamosi Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria.
    Mabao ya MC Alger yamefungwa na beki Ayoub Abdellaoui dakika ya 64 na mshambuliaji Soufiane Bayazid dakika ya 90'+5.
    Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Yanga ambayo ilianza michuano hiyo vibaya baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Al Hilal nyumbani, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, wakati MC Alger inapata ushindi wa kwanza kufuatia isare ya bila mabao ugenini na TP Mazembe Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Mchezo mwingine wa Kundi A utafuatia Jumapili usiku, Al Hilal Omdurman watakuwa wenyeji wa TP Mazembe kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Cheikha Ould Boidiya Jijini Nouakchott, Mauritania.​
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YACHAPWA 2-0 TENA LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top