KLABU ya Yanga imetangaza kumsajili kiungo anayeweza kucheza nafasi za ulinzi hususan beki wa kulia, Israel Patrick Mwenda (24) kutoka Singida Black Stars.
Mwenda aliyezaliwa Mwanza anakwenda kuungana na nyota watatu, kipa Abdutwalib Mshery na mabeki Kibwana Shomari na Dickson Job aliocheza timu ya taifa katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2017 nchini Gabon.
Kisoka Mwenda aliibukia Alliance FC ya Mwanza kuanzia timu ya vijana mwaka 2019 kabla ya kuhamia KMC mwaka 2020 ambako baada ya msimu mmoja akasajiliwa na vigogo, Simba SC alikocheza hadi Agosti mwaka huu alipohamia Singida Black Stars.
0 comments:
Post a Comment