WENYEJI, Singida Black Stars wametoka nyuman na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kengold FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida.
Kengold ilitangulia kwa bao la Hubert la winga Herbet Charles Lukindo dakika ya 25, kabla ya kiungo Muivory Coast, Josaphat Arthur Bada kuisawazishia Singida Black Stars dakika ya 46 na mshambuliaji Mkenya, Elvis Baranga Rupia kufunga la ushindi dakika ya 55.
Kwa ushindi huo, Singida Black Stars wanafikisha pointi 33 katika mchezo wa 15, ingawa wanabaki nafasi ya nne, wakati Kengold wanaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 wakibaki na pointi zao sita za mechi 16 sasa.
0 comments:
Post a Comment