TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na kiungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika ya 48 na beki mzawa, Kennedy Wilson Juma dakika ya 62.
Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 30 na kupanda nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 14.
Hali inazidi kuwa mbaya kwa Tanzania Prisons ikibaki na pointi zake 11 za mechi 14 na kushuka kwa nafasi moja zaidi hadi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.
0 comments:
Post a Comment