TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida.
Bao la Wekundu wa Msimbazi limefungwa na kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fabrice Luamba Ngoma dakika ya 42 akimalizia kona ya kiungo Muivory Coast, Jean Chjarles Ahoua kutoka upande wa kulia wa Uwanja.
Kwa ushindi huo, Simba SC wanakamilisha mechi zao 15 za mzunguko wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 40 na kuendelea kuongoza mbele ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 36 za mechi 14, wakiwazidi wastani wa mabao tu Azam FC.
Singida Black Stars baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 33 za mechi 16 sasa nafasi ya nne, mbele ya jirani zao Tabora United wenye pointi 25 za mechi 15.
0 comments:
Post a Comment