WENYEJI, KMC wamefanikiwa kutinga Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na benki ya NBC baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Black Six leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa na Daruesh Saliboko mawili, dakika ya tatu na la penalti dakika ya 17, Hance Masoud dakika ya 13, Rashid Chambo dakika ya 47 na Ally Shaaban dakika ya 79.
0 comments:
Post a Comment