WENYEJI, JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya bila mabao na Pamba Jiji ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kucheza ugenini, Pamba Jiji inayofundshwa na kocha mzoefu, Freddy Felix Minziro ilifanikiwa kuwadhibiti JKT na kuondoka na pointi moja katika vita yao ya kuepuka kushuka Daraja.
Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 17 na kusogea nafasi ya saba, ikiizidi wastani wa mabao Fountain Gate baada ya wote kucheza mechi 12, wakati Pamba Jiji inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 14 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 12.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu inaendelea muda huu Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba baina ya wenyeji, Kagera Sugar na Namungo ya Ruangwa mkoani Lindi.
0 comments:
Post a Comment