// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PACOME AFUNGA MAWILI YANGA YAICHAPA FOUNTAIN GATE 5-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PACOME AFUNGA MAWILI YANGA YAICHAPA FOUNTAIN GATE 5-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 29, 2024

    PACOME AFUNGA MAWILI YANGA YAICHAPA FOUNTAIN GATE 5-0


    MABINGWA watetezi, Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Yanga leo yamefungwa na  viungo Muivory Coast, Pacome Zouzoua Peodoh mawili, dakika ya 16 na 45’+1, Mudathir Yahya Abbas dakika ya 41, beki Jackson Katanga Shiga aliyejifunga dakika ya 52 na mshambuliaji Clement Francis Mzize dakika ya 88.
    Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 39 ikikamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, ingawa inabaki nafasi ya pili nyuma ya Simba yenye pointi 40 baada ya wote kucheza mechi 15.
    Fountain Gate baada ya kupoteza mchezo wa leo inabaki na pointi zake 20 za mechi 16 sasa, japokuwa inaendelea kubaki nafasi ya sita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PACOME AFUNGA MAWILI YANGA YAICHAPA FOUNTAIN GATE 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top