// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NDUGU WA MALAWI WAWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA KIKE AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NDUGU WA MALAWI WAWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA KIKE AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 05, 2024

    NDUGU WA MALAWI WAWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA KIKE AFRIKA


    WANASOKA wawili ndugu wa Malawi, Tabitha na Temwa Chawinga wameingia kwenyen orodha ya mwisho ya wachezaji wanaowania Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Mwanamke barani Afrika – wakichuana na Sanaa Mssoudy wa Morocco, Chiamaka Nnadozie wa Nigeria na Barbra Banda wa Zambia zitakazotolewa Desemba 16 Jijini Marrakech, Morocco.
    Tabitha anayechezea Olympic Lyon ya Ufaransa baada ya awali kuchezea PSG na Inter Milan na Temwa anayechezea Kansas City Current ya Marekani aliyojiunga nayo mwaka huu akitokea Wuhan Jianghan kufutaia awali kuchezea Kvarnsvedens IK ya Sweden – wote ni washambuliaji.
    Katika orodha ya mwisho ya wanaowania Tuzo za CAF kwa Wanawake kwa mwaka 2024 iliyotolewa leo, Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike Anayecheza Afrika imekutanisha wachezaji watatu wa AS FAR Rabat ya Morocco ambao ni Doha El Madani, Khadija Er-Rmichi na Sanaâ Mssoudy wanaochuana na nyota wawili wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Merveille Nanguji na Lacho Flora Marta.
    Mnigeria, Chiamaka Nnadozie wa Paris FC ya Ufaransa ndiye pekee achezaye Ulaya anayewania Tuzo ya Kipa Bora wa mwaka Mwanamke, akichuano na Fideline Ngoy wa TP Mazembe, Habiba Sabry wa FC Masar ya Misri, Khadija Er-Rmichi AS FAR Rabat na Andile Dlamini wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
    Kuna mchezaji mmoja tu anayecheza Ulaya anayewania Tuzo ya Mwanasoka Bora Chipukizi wa Kike, Mmorrco Lina Mokhtar Jamai wa Paris Saint-Germain anayechuana na Mmisri, Habiba Sabry wa FC Masar, Mmorroco Doha El Madani wa AS FAR Rabat, Mnigeria Chiamaka Okwuchukwu wa Rivers Angels ya kwa na Muafrika Kusini, Nthabiseng Majiya wa Mamelodi Sundowns.
    Mmorocco Lamia Boumehdi wa TP Mazembe ndiye Mwanamke pekee anayewania Tuzo ya Kocha Bora Soka ya Wanawake Afrika – akichuanana na Mmisri Ahmed Ramadan wa FC Masar, Mmorocco Mohamed Amine Alioua wa AS FAR Rabat, Mnigeria Christopher Musa Danjuma wa Nigeria U-20 na Muafrika Kusini, Thinasonke Phakamile Jessica Mbuli wa University of the Western Cape.
    Tuzo ya Timu Bora ya Taifa inawaniwa na Cameroon U-20, Morocco, Nigeria, Afrika Kusini na Zambia – wakati Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka inawaniwa na TP Mazembe, FC Masar, AS FAR Rabat, Edo Queens ya Nigeria na Mamelodi Sundowns.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDUGU WA MALAWI WAWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA KIKE AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top