MABINGWA watetezi, Yanga wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Dodoma Jiji mabao 4-0 katika jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na mshambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize mawili, dakika ya 19 na 38, kiungo Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 29 na mshamabuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 63.
Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 36, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na watani wa jadi, Simba SC baada ya wote kucheza mechi 14, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 16 za mechi 15 nafasi ya 11.
0 comments:
Post a Comment