// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); M-BET, HALOPESA KUWAZAWADIA MASHABIKI WA SOKA KUPITIA KAMPENI YA AMSHA AMSHA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE M-BET, HALOPESA KUWAZAWADIA MASHABIKI WA SOKA KUPITIA KAMPENI YA AMSHA AMSHA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, December 11, 2024

    M-BET, HALOPESA KUWAZAWADIA MASHABIKI WA SOKA KUPITIA KAMPENI YA AMSHA AMSHA

    MASHABIKI wa soka wa Tanzania, sasa wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha kupitia kampeni ya  Amsha Amsha iliyozinduliwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania na Halotel.
    Meneja Masoko wa M-Bet, Levis Paul aliema kuwa mbali ya zawadi ya fedha ya Sh50,000 kwa washindi wawili kwa siku, pia mashabiki wa soka wanaweza kujishindia fedha taslimu, simu janja, na televisheni za kisasa.
    Paul alisema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwazawadia wateja wao ambapo pia wanaweza kushindia fedha kwa kubashiri matokeo ya mechi katika ligi mbalimbali duniani.
    Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-BET Tanzania, Levis Paul (kushoto) na Afisa Masoko wa HaloPesa Aidat Lwiza wakionyesha kifurushi kilichojaa zawadi ambazo watazawadiwa wateja wao kupitia kampeni ya Amsha Amsha

    “Washindi wawili wa kila siku watajishindia Sh50,000, ambapo jumla ya Sh6,000,000 zimetengwa kwa kipindi hiki cha sikukuu,” alisema Paul. 
    Aliongeza kuwa kila mwisho wa wiki kutakuwa na droo maalum ambapo washindi wawili watajishindia simu janja ya Samsung A-Series yenye thamani ya Sh500,000.
    Zaidi ya hayo, wateja pia watapata nafasi ya kujishindia televisheni za kisasa aina ya Hisense zenye thamani ya Sh1.2 milioni kila moja, ambapo jumla ya televisheni nane zitatolewa katika kipindi cha miezi mitatu ya promosheni.
    Alisema kuwa shabiki wa soka anaweza kuingia kwenye droo kwa kujisajili kupitia tovuti yao, www.m-bet.co.tz, kuweka pesa kupitia HaloPesa, na kubeti kwa dau la kuanzia Sh2,000 ili kuingia kwenye droo.
    Kwa upande wake, Afisa Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza, alisema, “Tunafurahi kushirikiana na M-Bet kwenye promosheni hii. Lengo letu ni kutoa fursa kwa wateja kufurahia michezo ya kubashiri kupitia HaloPesa, ambayo ni njia rahisi na salama ya kufanya malipo. Promosheni hii itaunganisha burudani ya kubashiri na urahisi wa huduma za malipo ya simu.”
    Lwiza aliongeza kuwa promosheni hii itawawezesha wateja wa HaloPesa kufurahia huduma za M-Bet na kuingia kwenye droo za zawadi za kila siku, wiki, na mwezi.
    Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-BET Tanzania, Levis Paul (kulia) akizungumzia kampeni ya Amsha Amsha ambayo  wanashirikiana na kampuni ya simu ya teja na Halotel kupitia HaloPesa. Kushoto ni Afisa Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza.

    Wafanyakazi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-BET Tanzania na Halotel Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionyesha picha za zawadi mbalimbali katika kampeni ya Amsha Amsha.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: M-BET, HALOPESA KUWAZAWADIA MASHABIKI WA SOKA KUPITIA KAMPENI YA AMSHA AMSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top