WENYEJI, KMC wametoka suluhu na Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua, timu zote zilishambuliana kwa zamu na sifa ziwaendee makipa wa timu zote mbili za mabeki wao – kama si lawama kwa safu za ushambuliaji kukosa makali leo.
Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 15 katika mchezo wa 14 ingawa inabaki nafasi ya 11, wakati Mashujaa FC inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 13, nayo inabaki nafasi ya sita.
0 comments:
Post a Comment