// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIBU DENNIS SHUJAA…SIMBA YAIKANDA SFAXIEN 2-1 ‘KWA MKAPA’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIBU DENNIS SHUJAA…SIMBA YAIKANDA SFAXIEN 2-1 ‘KWA MKAPA’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 15, 2024

    KIBU DENNIS SHUJAA…SIMBA YAIKANDA SFAXIEN 2-1 ‘KWA MKAPA’


    WENYEJI, Simba SC wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezo wa mwisho mzunguko wa kwanza Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Shujaa wa Simba SC leo ni kiungo mshambuliaji, Kibu Dennis Prosper aliyefunga mabao yote mawili, dakika ya saba akimalizia pasi ya kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua na dakika ya 90’+9 akimalizia pasi ya kiungo mzawa, Yusuph Ally Kagoma.
    Mshambuliaji Mtunisia, Hazem Haj Hassen alianza kuifungia CS Sfaxien dakika tatu akitumia makosa ya beki Mcameroon, Che Fondoh Malone Junior kumrejeshea pasi fupi kipa wake, Mguinea Moussa Camara akaunasa mpira njiani na kufunga.
    Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi sita katika mchezo wa tatu na kujiweka sawa nafasi ya pili ikizidiwa wastani wa mabao tu na vinara, CS Constantine ya Algeria ambao wamecheza mechi mbili na wote wapo mbele ya Bravos do Maquis ya Angola yenye poimto tatu.
    Mabingwa wa zamani wa Kombe la Shirikisho wanakamilisha mechi tatu bila ushindi, wakifungwa zote pamoja na 1-0 kwa CS Constantine nyumbani na 3-2 kwa Bravos do Maquis nchini Angola.
    Mchezo mwingine wa Kundi A vinara CS Constantine watakuwa wageni wa Bravos do Maquis kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Novemba 11 Jijini Luanda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIBU DENNIS SHUJAA…SIMBA YAIKANDA SFAXIEN 2-1 ‘KWA MKAPA’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top