WENYEJI, Kagera Sugar wametoa sare ya bila mabao na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.
Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inafikisha pointi 10, ingawa inabaki nafasi ya 14 ikizidiwa pointi moja na zote, Pamba Jiji na Tanzania Prisons zinazofuatana nafasi ya 12 na 13 baada ya wote kucheza mechi 13.
0 comments:
Post a Comment