TIMU ya JKT Tanzania imefanikiwa kwenda Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Igunga United jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Wilson Nangu dakika ya 12, Nahodha John Bocco dakika ya 14, Mohamed Bakari mawili dakika ya 16 na 30 na Danny Lyanga dakika ya 68, wakati bao pekee la Igunga United limefungwa Joel Loya dakika ya 58.
MATOKEO YOTE MECHI ZA JANA KOMBE LA CRDB
Cosmopolitan 2-0 Nyota Academy, Mabatini Pwani
Polisi Tanzania 1-0 Bukombe Combine, Ushirika, Moshi
African Sports 1-1 (Penalti 2-3) Town Stars, TFF, Tanga
Stand United 2-0 Don Bosco, Kambarage, Shinyanga
Namungo FC 2-1 TANESCO, Majaliwa, Ruangwa
JKT Tanzania 5-1 Igunga United, Isamuhyo, Mbweni
0 comments:
Post a Comment