// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); FOUNTAIN GATE YAICHAPA COASTAL UNION 3-2 TANZANITE KWARAA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE FOUNTAIN GATE YAICHAPA COASTAL UNION 3-2 TANZANITE KWARAA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, December 13, 2024

    FOUNTAIN GATE YAICHAPA COASTAL UNION 3-2 TANZANITE KWARAA


    WENYEJI, Fountain Gate wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
    Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Burundi, Elie Mokono Eldhino mzaliwa wa Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 16, mshambuliaji William Edgar dakika ya 47 na kiungo Mghana, Nicholas Gyan kwa penalti dakika ya 54.
    Kwa upande wao Coastal Union mabao yao yamefungwa na kiungo Lucas Almeida Kikoti dakika ya 44 kwa mkwaju wa penalti pia na mshambuliaji Maabad Maulid Maabad dakika ya 79.
    Kwa ushindi huo, Fountain Gate wanafikisha pointi 20 katika mchezo wa 13 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya sita, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 16 za mechi 13 pia nafasi ya tisa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YAICHAPA COASTAL UNION 3-2 TANZANITE KWARAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top