WENYEJI, Azam FC wamefanikiwa kutinga Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Michuano inayodhaminiwa na benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Iringa SC leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo Mkongo, Yanick Litombo Bangala dakika ya 25, beki Mcolomboa, Yeison David Fuentes Mendoza dakika ya 45’+1, Sospeter Bajana dakika ya 65 na Daud Said dakika ya 74.
MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA CRDB BANK CUP
NOVEMBA 7, 2024
KMC 5-0 Black Six, KMC Complex, Mwenge
Pamba Jiji 1-0 Moro Kids, CCM Kirumba, Mwanza
Fountain Gate 2-0 Mweta Sports, tanzanite Kwaraa, Babati
Coastal Union 4-0 Stand FC, Sheikh Amri Abeid, Arusha
Azam FC 4-0 Iringa Sports, Azam Complex, Chamazi
Transit Camp 3-2 Gunners FC, Mabatini, Mlandizi
Biashara United 5-0 TRA FC, Karume, Ilala
Songea United 2-2 (Penalti 3-1) Kiduli FC, Maji Maji, Songea
Dodoma Jiji 1-1 (Penalti 4-5) Leo Tena, Jamhuri, Dodoma
Mtibwa Sugar 1-0 Greenland, Manungu Complex, Turiani
Singida Big Stars 2-0 Magnet FC, LITI, Singida
Mashujaa FC 3-0 Tukuyu Stars
NOVEMBA 6, 2024
Cosmopolitan 2-0 Nyota Academy, Mabatini, Mlandizi
Polisi Tanzania 1-0 Bukombe Combine, Ushirika, Moshi
African Sports 1-1 (Penalti 2-3) Town Stars, TFF, Tanga
Stand United 2-0 Don Bosco, Kambarage, Shinyanga
Namungo FC 2-1 TANESCO, Majaliwa, Ruangwa
JKT Tanzania 5-1 Igunga United, Isamuhyo, Mbweni
0 comments:
Post a Comment