WENYEJI, Azam FC wametoka nyuma kwa bao moja na kushinda mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Pascal Msindo dakika ya 36 na Iddi Suleiman 'Nado' mawili, dakika ya 63 na 71 baada ya JKT Tanzania kutangulia kwa bao la Said Ndemla dakika ya 13.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 36 katika mchezo wa 16, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi mbili mkononi.
Na wote wapo nyuma ya Simba SC inayoongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 37 baada ya kucheza mechi 14 kama Yanga.
0 comments:
Post a Comment