WENYEJI, Azam FC wametanua mbawa kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na winga Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 31 na mshambuliaji Msenegal, Alassane Diao dakika ya 90’+1 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 33 katika mchezo wa 15 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu.
Azam FC ipo mbele ya Singida Black Stars inayofuatia kwa pointi zake 30 za mechi 14, Simba SC pointi 28 na mabingwa watetezi, Yanga pointi 27 baada ya wote kucheza mechi 11.
Kwa upande wao Fountain Gate baada ya kupoteza mechi ya leo wanabaki na pointi zao 20 kufuatia kucheza mechi 14 na wanabaki nafasi ya sita.
0 comments:
Post a Comment