• HABARI MPYA

        Friday, November 15, 2024

        YANGA YAMFUTA KAZI GAMONDI NA MSAIDIZI WAKE MSENEGAL


        KLABU ya Yanga imeachana na kocha wake, Muargentina Miguel Angel Gamondi pamoja na msaidizi wake, Moussa N’Daw baada ya msimu mmoja na nusu wa kuwa timu hiyo.
        Yanga inaachana na Gamondi baada ya timu kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara wakifungwa 1-0 na Azam FC Novemba 2 na Tabora United 3-1 Novemba 7 zote Uwanja wa Azam FC Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
        Gamondi anaondoka Yanga akiiacha na mataji matatu aliyoikuta nayo, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama CRDB Bank Federation Cup.
        Zaidi Miguel Angel Gamondi atakumbukwa daima katika historia ya Yanga baada ya kuiongoza timu hiyo kuichapa Simba mabao 5-1 Novemba 5 mwaka jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: YANGA YAMFUTA KAZI GAMONDI NA MSAIDIZI WAKE MSENEGAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry