• HABARI MPYA

        Saturday, November 09, 2024

        YANGA SC YAHAMA CHAMAZI, SASA KUBANANA NA SIMBA UWANJA WA KMC

        KLABU ya Yanga umesema itautumia Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC Complex), Mwenge Jijini Dar es Salaam kwa mechi zake zijazo za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
        Awali, Yanga ilikuwa inautumia Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kwa mechi zake za nyumbani na maamuzi haya yanakuja baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Azam FC 1-0 na Tabora United 3-1.
        Mbali na wamiliki wa Uwanja, KMC timu nyingine ya Ligi Kuu inayotumia Uwanja wa KMC kama wa nyumbani ni Simba SC.

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: YANGA SC YAHAMA CHAMAZI, SASA KUBANANA NA SIMBA UWANJA WA KMC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry