Saturday, November 23, 2024

    TWIGA STARS YAPANGWA NA MABINGWA WATETEZI BANYANA WAFCON 2205


    TANZANIA imepangwa Kundi C pamoja na mabingwa watetezi, Afrika Kusini, Ghana na Mali katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) zinazotarajiwa kufanyika kuanzia Julai 5 hadi 26, mwaka 2025 nchini Morocco.
    Katika droo iliyopangwa jana ukumbi wa Mohammed VI Technical Centre mjini Salé, Morocco Kundi A linaundwa na wenyeji, Morocco, Zambia, Senegal na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati Kundi B linaundwa na Nigeria, Tunisia, Algeria na Botswana.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS YAPANGWA NA MABINGWA WATETEZI BANYANA WAFCON 2205 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry