• HABARI MPYA

        Sunday, November 03, 2024

        TANZANIA PRISONS YAWAKANDA KEN GOLD 1-0 SOKOINE


        TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya ndugu zao, Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. 
        Bao la Tanzania Prisons leo limefungwa na Jumanne Elfadhili Nimkaza kwa penalti dakika ya 52 na kwa ushindi huo inafikisha pointi 10 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya 12.
        Kwa upande wao Ken Gold waliopanda Ligi Kuu msimu huu wanabaki na pointi zao tano za mechi 11 sasa wakiendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAWAKANDA KEN GOLD 1-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry