TIMU ya Tabora United imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Dar es Salaam.
Mabao ya Tabora United leo yamefungwa na viungo washambuliaji, Mburkinabe Yacouba Sogne dakika ya 43 na mzawa, Offen Francis Chikola dakika ya 56.
Kwa ushindi huo, Tabora United wanafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya tano, wakati KMC inabaki na pointi zake 14 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechin 13.
0 comments:
Post a Comment