// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PAMBA YAZINDUKA NA KUICHAPA FOUNTAIN GATE PUNGUFU 3-1 BABATI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PAMBA YAZINDUKA NA KUICHAPA FOUNTAIN GATE PUNGUFU 3-1 BABATI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, November 05, 2024

    PAMBA YAZINDUKA NA KUICHAPA FOUNTAIN GATE PUNGUFU 3-1 BABATI


    HATIMAYE Pamba Jiji imeshinda mechi ya kwanza tangu ipande Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu huu baada ya kuwachapa wenyeji, Fountain Gate mabao 3-1 leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
    Haukuwa ushindi mwepesi, kwani Pamba Jiji ililazimika kutoka nyuma baada ya Fountain Gate kutangulia kupata bao, lililofungwa na kiungo Mkongo, Elie Mokono dakika ya 28.
    Pamba ikazinduka na kufunga mabao matatu mfululizo kupitia kwa nyota wake wazawa, washambuliaji, James Mwashinga akisawazisha dakika ya 31, kabla ya Saleh Masoud Nakibinge kufunga la pili dakika ya 45 na ushei na beki ambaye sasa anacheza kama winga wa kushoto, Ally Ramadhan ‘Oviedo’ kufunga la tatu dakika ya 86.
    Fountain Gate ilicheza pungufu kuanzia dakika ya 39 kufuatia mshambuliaji wake, Kassim Suleiman Hamisi kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kucheza rafu.
    Kwa ushindi huo, Pamba Jiji wanafikisha point inane katika mchezo wa 11, ingawa wanabaki nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu timu mbili zitateremka na mbili zinazofuatia zitakwenda kwenye mchujo wa kuwania kusalia Ligi Kuu.
    Kwa upande wa Fountain Gate baada ya kupoteza mchezo wa leo wanasalina na alama zao 17 wakiwa wamecheza mechi 11 sasa wakishika nafasi ya tano. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBA YAZINDUKA NA KUICHAPA FOUNTAIN GATE PUNGUFU 3-1 BABATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top