WENYEJI, Ken Gold wametoa sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Coastal Union walitangulia kwa bao la kiungo Mkenya, Hassan Abdallah Hassan 'Star Boy' dakika ya 42, kabla ya mshambuliaji Emanuel Steven Mpuka kuisawazishia Ken Gold dakika ya 87.
Kwa matokeo hayo, Ken Gold inafikisha pointi sita katika mchezo wa 12 na inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16, wakati Coastal Union inafikisha pointi 13 katika mchezo wa 12, nayo inabaki nafasi ya 10.
0 comments:
Post a Comment