// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DODOMA JIJI YAIBAMIZA KMC 2-1 JAMHURI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DODOMA JIJI YAIBAMIZA KMC 2-1 JAMHURI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, November 24, 2024

    DODOMA JIJI YAIBAMIZA KMC 2-1 JAMHURI


    WENYEJI, Dodoma Jiji wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
    Mabao ya Dodoma Jiji leo yamefungwa na winga Iddi Kipagwile kwa penalti dakika ya saba na mshambuliaji Paul Peter dakika ya 90’+1, wakati bao pekee la KMC limefungwa na Ali Shaaban dakika ya 87.
    Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 16 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya nane, wakati KMC inayobaki na pointi zake 14 za mechi 12 sasa inashukia nafasi ya tisa.
    Wakati huo huo: Mchezo kati ya Tabora United na Singida Black Stars uliositishwa leo baada ya dakika kadhaa kipindi cha kwanza Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora sasa utachezwa kesho asubuhi kama hali ya hawa itaruhusu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DODOMA JIJI YAIBAMIZA KMC 2-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top