• HABARI MPYA

        Monday, November 25, 2024

        AUSSEMS AONDOLEWA SINGIDA BAADA YA MECHI TATU BILA USHINDI


        KLABU ya Singida Black Stars imesitisha mikataba na makocha wake, Mbelgiji Patrick Aussems na msaidizi wake, Dennis Kitambi kufuatia timu kucheza mechi tatu mfululizo bila ushindi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
        Mara ya mwisho Singida Black Stars kushinda ni Oktoba 25 ilipoichapa Fountain Gate mabao 2-0 Uwanja wa CCM Liti mjini Singida.
        Baada ya hapo ilifungwa 1-0 na Yanga Oktoba 30 na sare mbili, 0-0 na Coastal Union Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na 2-2 na Tabora United leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: AUSSEMS AONDOLEWA SINGIDA BAADA YA MECHI TATU BILA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry