// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA PRINCESS YAITOA SIMBA QUEENS KWA MATUTA NGAO YA JAMII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA PRINCESS YAITOA SIMBA QUEENS KWA MATUTA NGAO YA JAMII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 02, 2024

    YANGA PRINCESS YAITOA SIMBA QUEENS KWA MATUTA NGAO YA JAMII

    TIMU ya Yanga Princess imefanikiwa kuingia Fainali ya michuano ya Ngao ya Jamii kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 na watani, Simba Queens Uwanja wa jioni ya leo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
    Yanga Princess walitangulia kwa bao la dakika ya kwanza tu la mshambuliaji wake chipukizi mzawa, Agness Palangyo, kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Kenya, Jentrix Shikangwa Milimu kuisawazishia Simba Queens dakika ya 88.
    Katika mikwaju ya penalty, kipa wa Mnigeria wa Yanga Princess, Rita Akarekor aliibuka shujaa baada ya kuokoa kuokoa penalty tatu, ikiwemo ya mwisho iliyopigwa na mchezaji mkongwe, mlinzi Fatma Issa Suleiman ‘Densa’.
    Sasa Yanga Princess watakutana na JKT Queens Jumamanosi katika Fainali hapo hapo Uwanja wa KMC, huku Simba Queens wakicheza na CEASIAA Queens kuwania nafasi ya tatu.
    Kwa upande wao JKT Queens walitangulia Fainali baada ya kuichapa CEASIAA Queens 7-0, Stumai Abdallah Athumani aking’ara Zaidi kwa kufunga hat trick.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA PRINCESS YAITOA SIMBA QUEENS KWA MATUTA NGAO YA JAMII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top