// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SINGIDA BLACK STARS WAICHAPA FOUNTAIN GATE 2-0 LITI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SINGIDA BLACK STARS WAICHAPA FOUNTAIN GATE 2-0 LITI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, October 25, 2024

    SINGIDA BLACK STARS WAICHAPA FOUNTAIN GATE 2-0 LITI

    TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain  Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Liti mjini Singida.
    Mabao ya Singida Black Stars leo yamefungwa na viungo Muivory Coast, Josaphat Arthur Bada dakika ya 54 na mzawa, Ayoub Reuben Lyanga dakika ya 65.
    Kwa ushindi huo, Singida Black Stars iliyo chini ya Mbelgiji, Patrick Aussems inafikisha pointi 22 katika mchezo wa nane na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya vigogo, Simba SC baada ya wote kucheza mechi nane.
    Kwa upande wao Fountain Gate baada ya kipondo cha leo wanabaki na pointi zao 16 za mechi tisa sasa nafasi ya nne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS WAICHAPA FOUNTAIN GATE 2-0 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top