// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YAPUNGUZA MWENDO LIGI KUU, SARE YA 2-2 NA COASTAL UNION MWENGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YAPUNGUZA MWENDO LIGI KUU, SARE YA 2-2 NA COASTAL UNION MWENGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, October 04, 2024

    SIMBA SC YAPUNGUZA MWENDO LIGI KUU, SARE YA 2-2 NA COASTAL UNION MWENGE

    VIGOGO, Simba SC wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
    Simba waliuanza vizuri mchezo huo na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza 2-0 kwa mabao ya beki na Nahodha wake, Mohamed Hussein 'Tshabalala' dakika ya 25 na mshambuliaji wake mpya, Mcameroon Christian Leonel Ateba Mbida kwa penalti dakika ya 40.
    Coastal Union walirejea na mipango mipya kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha mabao hayo kupitia kwa winga wake Mkenya, Hassan Abdallah Hassan dakika ya 47 na beki wa kushoto, Mkongo Hernest Briyock Malonga dakika ya 71.
    Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi 13 katika mchezo wa tano, wakati Coastal Union inatimiza pointi tano katika mchezo wa saba.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAPUNGUZA MWENDO LIGI KUU, SARE YA 2-2 NA COASTAL UNION MWENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top