// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA NA YANGA ZAWANIA TUZO YA KLABU BORA AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA NA YANGA ZAWANIA TUZO YA KLABU BORA AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 24, 2024

    SIMBA NA YANGA ZAWANIA TUZO YA KLABU BORA AFRIKA


    VIGOGO wa soka nchini, Simba na Yanga wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka Afrika baada ya kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.
    Watani hao wa hadi wanachuana na Al Ahly na Zamalek, zote za Mısri, Petro Atletico ya Angola, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Dreams FC ya Ghana, RS Berkane ya Morocco, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Esperance ya Tunisia.
    Wakati Simba ilitolewa na Al Ahly ya Mısri kwa jumla ya mabao 3-0, ikifungwa 1-0 nyumbani na 2-0 ugenini - Yanga ilitolewa na Mamelodi Sundwons kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya jumla ya 0-0.
    Al Ahly ndio walioibuka mabingwa baada ya kuichapa Esperance 1-0 ugenini na sare ya 0-0 nyumbani.
    Katika Nusu Fainali Al Ahly iliitoa Mazembe ikiichapa 2-0 Cairo baada ya sare ya 0-0 Lubumbashi na Esperance iliitoa Mamelodi kwa jumla ya mabao 2-0 ikishinda 1-0 nyumbani na ugenini. 
    Kwa Yanga huu ni mwaka wa pili mfululizo wanawania Tuzo hiyo ambayo mwaka jana ilichukuliwa na Al Ahly.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA ZAWANIA TUZO YA KLABU BORA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top