// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAMATTA AREJESHWA TAIFA STARS KWA AJILI YA MECHI NA DRC KUFUZU AFCON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAMATTA AREJESHWA TAIFA STARS KWA AJILI YA MECHI NA DRC KUFUZU AFCON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 01, 2024

    SAMATTA AREJESHWA TAIFA STARS KWA AJILI YA MECHI NA DRC KUFUZU AFCON


    KAIMU Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco amefanikiwa kumrejesha kikosini Nahodha Mbwana Ally Samatta ambaye alidhamiriwa kustaafu.
    Morocco amemjumuisha kwenye kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco.
    Taifa Stars watakuwa wageni wa DRC Alhamisi ya Oktoba 10 Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte Jijini Kinshasa, kabla ya timu hizo kurudiana siku tano baadaye, Oktoba 15 Uwanja Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Mara ya mwisho Samatta aliichezea Taifa Stars Januari 24, mwaka huu kwenye mechi ya Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 dhidi ya DRC Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo timu hizo zikitoka suluhu, 0-0 ambayo Samatta alimpisha Kokola Charles William M'Mombwa dakika ya 86.
    Makipa; Ally Salim (Simba), Zuberi Foba (Azam FC), Yona Amos (Pamba), Mohamed Hussein (Pamba FC).
    Mabeki; Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Pascla Msindo (Azam FC), Mohamed Hussein (Simba), Ibrahim Bacca (Yanga), Bakari Mwamyeto (Yanga), Dickson Job (Yanga), Abdulrazack Hamza (Simba), Haji Mnonga (Salford City, England),
    Viungo; Adolf Mtasingwa (Azam FC), Habib Khalid (Singida Black Stars), Himid Mao (Taalal El Geish, Misri) Mudathir Yahya (Yanga), Faisal Salum, Suleiman Mwalimu, Cyrpian Kachwele (Vancouver Whitecaps, Canada).
    Washambuliaji; Clement Mzizie (Yanga), Mbwana Samatta (PAOK FC), Kibu Dennis (Simba), NassOR Saadun (Azam FC) na Abdallah Said (KMC).  

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AREJESHWA TAIFA STARS KWA AJILI YA MECHI NA DRC KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top