MKONGWE Robert Lewandowski usiku wa jana alifunga mabao mawili kuiwezesha Barcelona kushinda 4-0 dhidi ya wenyeji, Real Madrid katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid, Hispania.
Mpoland huyo alifunga mabao yake mfululizo dakika za 54 akimalizia pasi ya Marc Casadó na 56 akimalizia pasi ya Alejandro Balde, wakati mabao mengine ya Barca yalifungwa na dogo Mspaniola Lamine Yamal dakika ya 77 na Mbrazil Raphael Dias Belloli Raphinha dakika ya 84.
Kwa ushindi huo, Barcelona inatanua uongozi wake kileleni mwa La Liga ikifikisha pointi 30, sita zaidi ya mabingwa watetezi, Real Madrid baada ya wote kucheza mechi 11.
0 comments:
Post a Comment