TIMU ya JKT Queens imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga Princess jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Hongera kwa mfungaji wa bao hilo pekee Donisia Daniel Minja kwa shuti la chini la mpira wa adhabu dakika ya 88 lililompita kipa Mnigeria wa Yanga Princess, Rita Akarekor licha ya juhudi zake za kuuchupia kulia kwake pembezoni kabisa mwa goli.
Katika mchezo uliotangulia wa kutafutab mshindi wa tatu, Simba Queens waliichapa CEASIAA Queens ya Iringa 4-0, mabao ya Asha Djafar mawili, dakika ya nne na 68, Satra Shamte aliyejifunga dakika ya 10 na Mnigeria Precious Christopher dakika ya 18.

0 comments:
Post a Comment