// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); FOUNTAIN GATE YAILAMBA KMC MABAO 3-1 TANZANITE KWARAA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE FOUNTAIN GATE YAILAMBA KMC MABAO 3-1 TANZANITE KWARAA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, October 21, 2024

    FOUNTAIN GATE YAILAMBA KMC MABAO 3-1 TANZANITE KWARAA


    WENYEJI, Fountain Gate wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
    Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Dickson Ambundo dakika ya nane, Suleiman Mwalimu dakika ya 23 na William Edgar dakika ya 59, wakati bao pekee la KMC limefungwa na Andrew Vincent dakika ya 47.
    Kwa ushindi huo, Fountain Gate inafikisha pointi 16 katika mchezo wa nane na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tatu na Singida Black Stars ambayo imecheza mechi saba.
    Wote wapo mbele ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 15 za mechi tano, Azam FC wenye pointi 15 pia za mechi nane na Simba pointi 13 za mechi sita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YAILAMBA KMC MABAO 3-1 TANZANITE KWARAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top